HUYU Ndiye Ruge Ninayemfahamu...!!!!


Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Hata kama kwa ubinadamu wetu tutatashindwa kusimama na huyu ndugu hususan kwa kipindi hiki yupo Mungu aliye hai atamtetea. 

Ndio, Hakuna binadamu asiye na mapungufu, Ruge kama binadamu inawezekana ana mapungufu yake lakini katika hili suala la Clouds Vs "Yule Bwana" kwa binadamu mwenye akili za kawaida tu utakubaliana nami kwamba Ruge ameonyesha hekima na busara ya kiasi cha juu sana.

Alichoamua Kukisimamia Ruge ni kusema UKWELI, Ukweli kwamba "Yule Bwana" alikosea, pamoja na kwamba walikuwa marafiki lakini Ruge aliamua kusimama katika misingi ya ukweli, misingi ya kikazi, Kwamba "Yule bwana" alikosea. Kuna vitu wala havihitaji degree kuvielewa, yaani kule tu kwenda pale tena usiku tena na silaha bila mhusika kujua, na bila warrant ni kosa kisheria.

Leo baada ya kumsikia Ruge akijibu shutuma za "Yule Bwana" nimejisikia amani sana, Maana badalaa ya kujibu kwa jaziba, kwa matusi, kwa mhemko, Ruge kajishusha kaongea kwa ustaarabu kama binadamu, Pamoja na kuambiwa hana akili, anaimba ngonjera, na maneno mengine mengi ya kuudhi lakini jamaa kajibu ki proffesional na kwa unyenyekevu. U have my respect brother.

Mi nafikiri kama taifa kama tunakuwa na viongozi wa namna hii, ambao wanashindwa kuwa na akiba ya maneno na kuongea tu kama vijana wa mtaani bila kuangalia kuwa kuna watu wengi sana tunawaangalia ili kujifunza kwao, tutakuwa tunaelekea pabaya sana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad