HUZUNI: Hili Neno "KATA" la Mheshimiwa Rais Limezua na Linazua Hali Mbaya Sana Nchini..!!!


Siwezi kumuita Rais wetu Mh. J.P Magufuli kama Dikteta au mwenye Ukatili na asiyewajali watu wake ila kuna kauli zake zimekuwa zikisababisha mateso makubwa sana kwa wananchi wake.

Ukiacha zile za wakati wa Njaa na Tetemeko la ardhi.

Mfano mkubwa mzuri ni hili neno alilotoa kuhusu ukataji wa umeme kuwa endapo mwananchi yeyote wa mahali popote atakuwa/watakuwa hawajalipia umeme basi TANESCO wasihoji chochote bali wakate umeme. 

Amekuwa akisema kuwa hata kama ni Ikulu haijalipia umeme (kitu ambacho kamwe hakiwezekani) basi wakate ilihali umeme haukatiki huko asilani.

KINACHOUMIZA ZAIDI, leo Mbunge wa Morogoro kupitia CHADEMA ameelezea hali inayosikitisha na kuhuzunisha sana kuwa Wafungwa (Wanaume, Wanawake na Watoto) wa magereza ZOTE za mkoani morogoro wanaishi katika giza tororo kisa Umeme umekatwa huko.

Hali hiyo imekuwa ikisababisha hata wafungwa watoto kubakwa na kulawitiwa, wanawake kubakwa na kupata mimba kiholela.

Na isitoshe mazingira ya magereza ni magumu sanaa kwa binadamu yeyote kuishi.

Hivi sio serikali inayopaswa kulipia umeme wa magereza? Au ni hao wafungwa?

Ni kwanini Mh. Rais asifute hii kauli yake kwa sehemu kama hizi?

Je wananchi wa maeneo haya wanamchukuliaje Mh. Rais?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad