Jambazi aliyeuawa na Askari Dar alikuwa akisema "Allahu Akbar, Allahu Akbar"


Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, , Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, jambazi aliyeuawa juzi katika eneo la Kurasini, Manispaa ya Temeke, na wenzake wawili kutoroka, alikuwa anataka kupora Sh. milioni 320 kutoka katika gari la kampuni ya G4S lililokuwa likizisambaza kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) za CRDB.


Fedha hizo zilikuwa kwenye gari lenye namba za usajili T155 DCB aina ya Nissan mali ya kampuni ya ulinzi ya G4S huku likisindikizwa na askari wawili wa kikosi cha FFU.


Alisema wakati wahudumu wa G4S wakisambaza fedha, mmoja wa watu waliokuwa katika bodaboda hizo ghafla aliruka na kumvamia askari kwa lengo la kumpora silaha ili kufanikisha zoezi la uporaji wa fedha hizo. Alisema kuwa baada ya kitendo hicho jambazi huyo aliamriwa asimame lakini alikaidi na ndipo alipopigwa risasi iliyomjeruhi mguuni na nyingine tumboni kisha aliishiwa nguvu na kusika akitamka " Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar"

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo anabaki kuwa muhalifu lakini ni muislamu ambae anajaribu kutoa shahada kabla umauti kumfika kwa sababu ameshaishiwa nguvu nawaomba waislamu wenzangu tusimchezee Allah.

    ReplyDelete
  2. Hakuna ubaya KUSEMA ALLAHU AKBARI.UKISEMA MUNGU MKUBWA KUNA TATIZO?WACHENI FITINA ZA KIDINI.KILA DINI INAWAASI WAKE .KWANI HAKUNA WAISLAMU WALEVI,WAZINIFU.WAIZI?WAKO WENGI TU.SASA WEWE ULIEMSIKIA AMESEMA HIVYO UMETAFSIRI NINI?ANGESEMA HARE KRISHNA UNGEELEZEA MEDIA?
    NYOKONYOKO HIZO NDIO ZINAZOLETA FITINA BAINA YA DINI.TUWENI WAANGALIFU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad