JINGINE Jipya :Serikali Yakanusha Uzushi Kuhusu DR Mwakyembe

Kupitia mitandao ya kijamii zilienea uzushi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua zuio la Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliyevitaka vituo vya redio na televisheni kutokuzisoma habari nzima katika dondoo za magazeti. Wizara hiyo imekanusha uvumi huo kama ifuatavyo:

Tarehe 03 Mei, 2017 kupitia mitandao ya kijamii ulienezwa uzushi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua zuio la Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliyevitaka vituo vya redio na televisheni kutosoma habari nzima katika dondoo za magazeti.

Tunapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi uliotungwa kwa dhamira ovu kwani Mhe. Rais hajatoa tamko, maagizo wala maelekezo yoyote kuhusu maelekezo yenye nia njema yaliyotolewa na Mhe. Dkt. Mwakyembe.

Umma unakumbushwa kuwa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni, 2015 kinakataza na kutoa adhabu kali ikiwemo kifungo jela kwa wanaoeneza taarifa za uongo. Katika uzushi huu hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Kama ilivyokuwa kaulimbiu ya Siku ya Uhuru wa Habari iliyoadhimishwa jana, na pia alivyosisitiza Waziri Mwakyembe kwa wadau jijini Mwanza, moja ya nguzo kuu ya uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza ni ukweli. Tuitumie mitandao ya kijamii kwa faida na si kutangaza uongo na uzushi.

Siku ya maadhimisho ya sherehe ya vyombo vya habari, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo alipiga marufuku vituo vya redio na runinga kusoma habari nzima katika magazeti na kuamuru kusoma kichwa tu cha habari

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad