KAMANDA Sirro Hili Genge la Polisi Vibaka Unalitambua..!!?


Naamini hapa kuna wadau mbali mbali ikiwepo hata watu wakaribu au wanaofanya kazi chini ya kamanda siro .

Jana usiku kuna kundi la polisi lilivamia kibamba usiku wa manane kwenye mida ya saa nane usiku kwenye makazi ya watu na kuwanyanyasa ikiwa na kuiba fedha. 

Walikuwa wakifika wanagonga mlango ukifungua watu wote mnatakiwa kutoka nje hata kama ni nyumba ta wapangaji wote mnatolewa nje na kulazwa chini harafu wao wanaingia ndani na kuanza kusachi watapekua kila mahali na vyakubeba vitabebwa hasa pesa ndio haziachwi hapo.

Wanavunja mali za watu kama makabati yanavunjwa,milango inavunjwa tena milango inavunjwa na risasi za moto.

Wakigonga ukakataa kufungua wanavunja mlango na wakiingia ndani unachezea kichapo sana.
Risasi za moto zinapigwa hovyo usiku mpaka ndani kwenye makazi ya watu usiku watu wamelala tena na watoto wadogo wagonjwa lakini wao wanapiga tuu kwanza wengi wamelewaa.

Madai yao makuu wanadai wenzao wana uliwa sisi raia tunafurahia na ndio tunawaficha hao majambazi.

Kwa style hii wanayoitumia polisi ni ngumu sana kupata ushirikiano kutoka kwa raia wema.

Pesa zetu mnazichukua kinguvu mnaharibu mali zetu harafu mnataka tuwape ushirikiano?

Haya mambo ndio yanalichafua sana jeshi letu na kuweka uhasama kati ya polisi na raia wake.

Tunakuomba sana kamanda siro ulitolee ufafanuzi jambo hili.

Polisi wanatuonea sana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad