KAMANDA Sirro ni Mtu Pekee Anayefahamu Vyema Mauaji Yanayotokea Kibiti na Ikwiriri na Huenda Akawa na Majibu Yake..!!!


Mwaka 2012, Huko Ikwiriri wakati wa mapigano ya wakulima na wafugaji, aliyekuwa kamanda wa operesheni maalumu wa jeshi la polisi SACP Simon Sirro alitumwa kwenda kuweka mambo sawa.

Sirro akazungumza na wakulima, wafugaji, viongozi na polisi wa ikwiriri, lakini cha ajabu kidogo(kwa viongozi wa Tanzania), Simon Sirro alifanya jambo nadra kulifanya kwa viongozi wa kiafrika.

Akitoa majumuisho ktk mkutano wa hadhara akawatuhumu jeshi la polisi wa Ikwiriri Kuwa ndo chanzo cha mgogoro huo, kwani wamekuwa wakichukua "maziwa" kwa wafugaji na kusababisha kutotenda haki.

Akaendelea kuwalaumu polisi kuwa wanapaswa kutenda haki na "hali hiyo ikiendelea italeta shida na shaka siku za mbele".

Leo ni miaka mitano tumeona utabiri wa Simon Sirro, Mauaji ya polisi, viongozi wa chama dola na serikali wakiwa ni walengwa zaidi.

Hata ukweli upingwe vipi ila kwa sura ya nje Kibiti na Ikwiriri Kuna tatizo kubwa, huenda kuna kundi linalipa kisasi kwa uonevu walioupata mahala.

Kwa sasa ni mtu mmoja tu anaweza kutumia akili, uwezo na busara zake kuweka mambo sawa Kibiti, ni kamanda wa polisi wa mkoa wa DAR ES SALAAM wa sasa ndugu yangu Simon Sirro.

Nina hakika hata jeshi la polisi likiamua kufanya reform na likafanya mapinduzi ya kimuundo na kiutawala ili kujiweka ktk hali ya kukwepa lawama na chuki dhidhi yake kama raia kubambikiwa kesi, kujiingiza ktk siasa, matumizi makubwa ya nguvu, changamoto za ndani ya jeshi nk. huenda huyu bwana akaweza kuwa ni kiongozi wa mabadiliko hayo.

By Shukuru Ngonyani wa JF

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad