Kanye West ashangaza mashabiki wake, baada ya kafuta akaunti zake zote

Boss wa kampuni inayotengeneza mavazi ya Yeezy ,ameushangaza ulimwengu kwa kufuta akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Kanye ameamua kufuta akaunti yake ya Instagram pamoja na ile ya Twitter. Kufutwa kwa akaunti za rapa huyo kulianza kujulikana siku ya jana baada ya mashabiki zake kushangaa kutomuona kila walipokuwa wakimtafuta kwenye mitandao hiyo.

Mr. West ameamua kujiweka katika maisha ya kawaida hasa kwa upande wa kuonyesha kila anachofanya kupitia mitandao tangu alipotoka hospital mnnamo mwaka jana baada ya kupata stress za kupindukia na kushindwa hata kufanya shows.

Kwa sasa Kanye na Kim wameamua kubadilisha mfumo wa maisha kwa kutopendelea kuonyesha mali zao kwa kuzinadi katika mitandao ya kijamii.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad