KESI ya Wema Sepetu ya Kukutwa na Madawa ya Kulevya Yafikia Hatua Hii Mahakamani..!!!


Malkia wa filamu , Wema Sepetu, Jumanne hii amepanda tena katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Dar es salaam, kusikiliza kesi ya tuhuma za kutumia na kukutwa na madawa ya kulevya, ambapo upande wa Jamhuri umekamilisha upelelezi wa kesi inayomkabili msanii huyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ameahirisha kesi hiyo mpaka June 1, mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza maelezo ya awali ya upelelezi huo.

Muigizaji huyo, ambaye yupo nje kwa dhamana baada kusota mahabusu kwa siku 7, anadaiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake, kufuatia msako mkali wa kupambana na dawa za kulevya uliofanywa na ofisi ya mkoa wa Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad