Ikiwa ni siku mbili tu zimepita baada ya Simba kutiliana saini kandarasi ya udhamini na kampuni ya SportPesa, mdau wa klabu hiyo Mohammed ‘MO’ Dewji amekuja juu na kutaka kurejeshewa fedha zake TZS 1.4 bilioni baada ya klabu hiyo kuvunja makubaliano waliyokuwa wameafiki.
MO amesema kuwa anataka kulipwa fedha hizo ambazo alizitumia kuwalipa mishahara wachezaji wa Simba tangu mwaka jana.
Uamuzi huu ameutoa baada ya klabu hiyo kuingia makubalino ya udhamini na kampuni ya SportPesa pasi na kumshirikisha yeye ikiwa ni kinyume na makubaliano.
Mei 12, 2017, uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, ulisaini kandarasi ya udhamini wa miaka mitano na Kampuni ya SportPesa yenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.
Katiba barua aliyoandika MO, amesema kuwa Simba wamekiuka makubaliano waliyokuwa wamefikia kwamba, atoe fedha kwa makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa, na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba, inabidi wakae meza moja viongozi na yeye na hiyo kampuni ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba. Lakini katika kandarasi ya SportPesa, MO amesema hakushirikishwa.
Simba tayari ilishaanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.
Mrudishieni hela zake
ReplyDelete