KIMENUKAA..Jaji Mkuu Ampeleka Lissu Mahakamani..!!!


Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimepanga kwenda mahakamani kupata ufafanuzi wa kisheria kuhusu nafasi ya Jaji Mkuu.

Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema Baraza la Uongozi la chama hicho katika kikao chao kilichofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma, wameamua kuwa na kauli moja ya kurudisha utawala wa sheria na hawawezi kukaa kimya wakati mambo yanakwenda ndivyo sivyo.

“TLS tumeamua kufungua mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania kuhoji uhalali wa kikatiba wa Rais John Magufuli kushindwa hadi sasa kuteua kiongozi mkuu wa Mahakama ya Tanzania yaani Jaji Mkuu,” alisema Lissu.

Alisema kuwa baraza lao linaamini kuwa, Rais Magufuli anakiuka Katiba ya nchi ijapokuwa ana mamlaka kwa mujibu wa ibara ya 118 (4) inayomruhusu kuteua Jaji Mkuu iwapo itatokea nafasi hiyo kuwa wazi.

Alisema Kaimu Jaji Mkuu ni nafasi ya muda inayoshikiliwa na mtu mwenye sifa za kuwa Jaji Mkuu kabla haijajazwa na Jaji Mkuu kamili, lakini wanashangazwa na kauli aliyoitoa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi bungeni hivi karibuni kuwa mamlaka ya kukaimu hayana kikomo cha muda.

Pia, alisema wamepanga kuitisha mdahalo wa nchi nzima ambao utashirikisha viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, wasomi, wanataaluma na waliokuwa wajumbe wa Tume ya Katiba ili kujua mustakabali wa suala hilo.


Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu nae hana kazi za kufanya kwa sasa, nafikiri bora awe wakili wa wenye vyeti feki kwa sasa, maana ndio habari ya mujini

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad