Kufuatia ajali iliyotokea jana Mkoani Arusha na kuua watu zaidi ya 30, Chama Cha Mapinduzi kimetuma salamu zake za rambirambi na pole na kuongeza kuwa msiba huo wameupokea kwa masikitiko makubwa sana
Salamu hizo zimetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndg, Humphrey Polepole na kusema kuwa Chama Chama Mapinduzi kimepokea taarifa za ajali na vifo hiovyo kwa masikitiko makubwa kwa kuwa wanafunzi hao walikuwa katika safari ya kujiimarisha kiitaluma ili kutimiza malengo yao na
"Taifa limepoteza raia wema na nguvu kazi ya sasa na baadae. Chama kinatambua kuwa safari hiyo waliyokuwemo watoto hawa ilikuwa sehemu ya kuwaimarisha kitaaluma ili kutimiza ndoto zao maishani"- Humphrey Polepole
Aidha Katibu Mkuu wa Chama hicho Comrade Abrahman Kinana ameungana na Watanzania wote kupitia msiba huo na kusema kwamba
"Licha ya kwamba wapendwa wetu wametangulia mbele za haki , wataendelea kubaki katika kumbukumbu zetu daima na tunamuomba Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina. Tunawaombea Kupona haraka majeruhi wote waliotokana na ajali hiyo"- Abrahman Kinana.
Ajali hiyo imetokea jana Mkoani Arusha, Wilayani Karatu baada ya basi walilokuwa wamepanda wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent jijini Arusha walipokuwa wakienda kufanya mtihani wa ujirani mwema katika shule ya Tumaini kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo eneo la Rhotia Marera, ambapo limeua zaidi ya watu 30 wakiwepo wanafunzi, waalimu na dereva wa basi hilo.