KINANA Aibukia Arusha, Ateta na Lowassa, Mbowe..!!!


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana jana alionekana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva wa Shule ya Msingi ya Lucky Vicent waliofariki katika ajali ya gari Aprili 6.

Na kilichovuta macho ya wengi ni kuonekana akizungumza na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Kinana hajaonekana hadharani tangu kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Machi 12 mjini Dodoma.

Na maswali yalipoanza kuhusu kutoonekana kwake, Rais John Magufuli alisema “amemtuma India kwenda kutibiwa.

Jana, Kinana, ambaye amewahi kuwa mbunge wa Arusha na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, alionekana mjini hapa na alitumia muda mwingi kusalimiana na watu waliokuwa wakimfuata.

Kinana alifika uwanjani akiwa kwenye gari la ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha na alipanda moja kwa moja jukwaa kuu na baadaye alipata muda wa kusalimia mamia ya watu waliokuwa wamefurika katika uwanja huo.

Wakati shughuli za kuaga miili ikiendelea, Kinana aliteta kwa dakika chache na Lowassa aliyekuwa ameongozana naye.

Lowassa alisikika akimuuliza Kinana kuhusu afya yake na alijibiwa na katibu mkuu huyo wa CCM kuwa anaendelea vizuri. Wawili hao waliendelea na mazungumzo, huku wakipigwa picha.

Baadaye Kinana alizungumza na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia alimpa pole.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi jana kuhusu hilo, alisema: “Nitafute tutazungumza.”

Wakati huohuo, zaidi ya waombolezaji 100 walizimia wakati wa ibada ya kuaga miili hiyo.

Mmoja wa madaktari wa taasisi ya Msalaba Mwekundu ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema wamepokea watu watatu waliokuwa na hali mbaya akiwamo mtu huyo ambaye awali alidhaniwa kufa na baadaye akazinduka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad