Kundi la wapiganaji wa Islamic State (IS) limevamia mji wa Malawi ambao upo kusini mwa kisiwa cha Mindanao nchini Ufilipino.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Ufilipino imeeleza kuwa zaidi ya siku mbili wanajeshi wa nchi hiyo wamekuwa wakifanya mashambulizi ya anga katika mji wa Marawi, ambao umevamiwa na wanamgambo wa IS.
Chanzo cha mapambano hayo ni baada ya wanajeshi wa Ufilipino kuvamia nyumba moja ikimtafuta Kiongozi wa IS nchini Ufilipino, Isnilon Hapilon na kiongozi wa kundi la Abu Sayyaf.
Wanajeshi Takriban na Polisi 40 wameripotiwa kuuawa kwenye mapambano ya kurushiana risasi, huku maelfu ya raia kukimbia makazi yao.