Ndani ya kipindi cha miaka mitatu mtandao huo umeongeza watumiaji kwa kasi kubwa na inakadiriwa kila siku zaidi ya mtu mmoja hujiunga na mtandao.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na mtandao huo, kila mwezi idadi ya watu iliongezeka hadi bilioni 1.94, ambao watu bilioni 1.3 huutumia kila siku.Kampuni hiyo ya Kiteknolojia iliyo na makao makuu yake nchini Marekani, iliripoti faida za takriban dola bilioni 3 katika robo ya kwanza ya mwaka, ikiwa ni ongezeko la asilimia 76 kwa mwaka.
Siku ya Jumatano, mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Mark Zuckerberg, alitangaza kwamba atawaajiri watu 3000 zaidi kuweka maudhui ya wastani katika mtandao huo. Akizungumza baada ya ripoti hiyo ya matokeo, Zuckerberg alisema kwamba idadi ya watumiaji wake wameipatia Facebook fursa ya kupanua jukumu la mtandao huo, kuanzisha runinga, afya na siasa.
Robo ya idadi ya watu duniani inatumia facebook kila mwezi huku watumiaji wapya wakitoka nje ya bara Ulaya na Marekani Kaskazini. Hata hivyo imeonya kwamba ukuwaji wa mapato ya matangazo huenda ukashuka.