LEMA Afunguka Makubwa Kuhusu Unyanyasaji Unaofanyika Huko Magerezani..


Kambi ya rasmi ya upinzani bungeni imeitaka serikali kuhakikisha inalionya Jeshi la Magereza kuacha mara moja vitendo vya udhalilishaji kwa wafungwa unaofanywa na maaskari wakati wa ukaguzi pindi watuhumiwa wanapotoka mahakani.

Akisoma hotuba ya upinzani Waziri kivuli wa Mambo ya nje, Mh. Godbless Lema amesema kuwa ukosefu wa vifaa vya kisasa ndio chanzo cha udhalilishaji hivyo hali inayowafanya wafungwa kuvuliwa nguo hadharani na kukaguliwa kipindi wanapotoka mahakamani kitu ambacho ni udhalilishaji wa wa kibinadamu. "Wafungwa na mahabusu kuvuliwa nguo siyo vitendo vya kibinadamu ni utekelezaji wa mikakati ya kishetani. Kitendo hiki ni utekelezaji wa mikakati ya kishetani wazee na vijana kuvuliwa nguo na kukusanywa uchi na kukaguliwa hadharani, hata askari wanaofanya hivyo husababishiwa na huzuni bila sababu. Serikali inapaswa kununua vifaa vya ukaguzi maalumu ambavyo ni vya kisasa na haviwezi kuvunja utu. lakini pia kuna unyanyasaji ambao unatekelezwa na askari na kanuni mbovu za uendeshaji wa majeshi ya magereza"- Lema alifunguka.
Aidha katika hotuba hiyo iliyosomwa na Lema imeitaka serikali itimize vyema sheria ya Parole na kuwaachia huru wafungwa waliokaa magereza muda mrefu waachiliwe kwani hawawezi tena kufanya uhalifu. "Serikali iwaachie huru wafungwa waliokaa muda mrefu magereza wanautamani sana uhuru. ni vyema serikali ikaangalia jinsi ya kuwapa uhuru na kuachana na wale wafungwa wa vifungo vya muda mfupi. Kama mtu ana miaka 65 amekaa magereza miaka 25 akiachiliwa hawezi kwenda kufanya uhalifu tena. tunaiomba serikali iweze kuwaachia wafungwa wote waliofungwa toka awamu ya Nyerere mpaka awamu ya nne ya Mh. Kikwete kwa kuzingatia sheria ya Parole"- aliongeza Lema.
.
JE UNAMUUNGA MKONO LEMA AU UNAMPINGA????.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad