LIFAHAMU Kundi la Lazarus.. Kundi Tishio Duniani kwa Kuingilia na Kudukua Mifumo ya Kompyuta...!!!


Kundi la Lazarus ndilo kundi lenye kuheshimiwa zaidi kwa sasa duniani kwa kuwa na uwezo wa hali ya juu kabisa wa kuingilia mitandao mbalimbali na nyeti na kisha kudukua taarifa mbalimbali.

Pia kundi hilo la Lazarus linasadikiwa kuhusika na uingiliaji mitandao ya kibenki, usafiri na habari na kisha kuvuruga taratibu za uendeshaji mifumo hiyo.

Kundi la Lazarus wanajulikana kwa kutumia mtindo wao uitwao “Shadowy Hacking Collective” ambapo wanatumia msimbo au “codes” maalum kuingilia mifumo ya kompyuta.

Mwaka 2014 Lazarus waliingilia mifumo ya kampuni ya Sony ambayo inatumia programs za windows na kusababisha kutotolewa kwa filamu ya kichekesho iitwyo INTERVIEW ambayo ilikusudia kumwonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini .

Wakitumia jina lingine la Guardians of Peace kundi hili walianza kutoa hadharani taarifa za barua pepe, taarifa binafsi na taarifa mbalimbali za ndani.

Wakitoa sababu za kuingilia studio za kampuni ya Sony zilizoko mjini Hollywood, kundi la Guardian of Peace walidai kwamba walifanya hivyo ili kulipa kisasi kutokana na matengenezo ya filamu hiyo ya INTERVIEW.

Hata hivyo baadae raisi wa Marekani wakati huo Barak Obama akaomba radhi wapenzi wa filamu kwa kuwaambia kwamba kulikuwa na makosa fulani ya kiufundi na kuonekana kuwatumia lawama nchi ya Korea Kaskazini ambayo nayo ilikanusha kuhusika na udukuzi huo na kusema kwamba ni CIA na washirika wao ndiyo walikuwa wakipanga njama za kumuua kiongozi wa taifa hilo.

Kundi la Lazarus halikuishia hapo katika kampeni zake za kuangamiza mifumo ambayo haina ulinzi wa kutosha dhidi ya mitandao. Mwezi February mwaka 2016 kundi la Lazarus waliingilia mifumo ya kibenki nchini Bangladesh na kuchukua fedha kiasi cha dola milioni 100.

Kitendo hicho kiliendelezwa hadi katika nchi za Vietnam na Phillipenes ambapo misimbo au “codes” za Lazarus za Trojan.Banswift zilitumika na na program hasidi au “malware” ilojulikana kwa jina la Backdoor.Contopee iligundulika kuwa ilitumiwa na Lazarus.

Kampuni kubwa ya Symantec ya Marekani ikitumia watafiti wake na wachunguzi mbalimbali, walitoa taarifa kadhaa kuonyesha jinsi msimbo inavyotumiwa ambapo ilionekana inatokea sehemu moja.

Pia kuthibitisha hayo mtafiti na muanzilishi wa Anti-Virus software ya MacAfee bwana John MacAfee nae amethibitsha kwamba kundi hilo lipo na limegawanyika sehemu mbalimbali duniani.

Baada ya shambulizi la siku ya Ijumaa, serikali nyingi duniani, taasisi na makampuni mbalimbali zimetahadharishwa juu ya uwezekano wa kuwepo kwa mashambulizi zaidi katika mifumo na mitandao ambayo haiko salama.

Kwa mujibu wa taasisi ya usalama wa mitandao NCSC na ile ya ulinzi wa taifa ya Marekani ya NSA wadukuzi wamepanga kushambulia vifaa vya kiteknolojia ambavyo huunganishwa katika mitandao ya internet kama simu ya mkononi au smartphones, televisheni au Smart TV, kompyuta mpakato, tablets na saa za mikononi zenye simu au smartwatch.

Vifaa vingine na mitambo ni kama vile webcam, taa za kuongozea magari yaani traffic lights, mitambo ya kufua umeme, taa za barabarani, majokofu ya Samsung ambayo yana tumia teknolojia maalum ya kuyaongoza, mifumo ya camera za ulinzi ya CCTV na hata kamera maalum za kuwaangalia watoto wachanga au Video baby monitors vifaa ambavyo zinaunganishwa katika mitandao ya internet.

Mashambulizi ya kutumia ransomware katika vifaa tajwa hapo juu yatasababisha matatizo makubwa kwa watengenezaji hali itakayopelekea ugumu wa idara za usaidizi au support katika kutoa msaada kwa wateja kujaribu kufungua vifaa hivyo endapo vitadhurika na kirusi cha Ransomware.

Serikali mbalimbali duniani zimechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya dharura na pia kuchukua hatua za tahadhari kulinda miundombinu muhimu.

Kwani kundi la Lazarus halijulikani na pia hakuna anaefahamu kundi hili linejipanga vipi kwa sasa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad