Maalim Seif katika Mahojiano na Clouds asubuhi hii amesema kuwa hawezi kamwe kukaa meza moja na Profesa Lipumba.
Amesema ni bora akae na CCM kwani anawajua kabisa ni adui lakini si msaliti Lipumba na kusisitiza "Mimi siwezi kukaa na Msaliti"
Akaulizwa kuwa mbona hapo nyuma aliwahi kuwa na uhasama wa wazi kabisa na Sumaye lakini baadaye alikaa naye meza moja UKAWA?
Akasema uhasama wake na Sumaye ulikuwa wa tofauti za kichama na alimjua wazi kuwa ni adui kwani alikuwa CCM lakini kwa Lipumba ni tofauti kwani ni msaliti.
Maalim Seif: CUF kwa sasa inaendeshwa kwa pesa za michango ya wanachama. Matajiri hawaji CUF kwani wakiwajua TRA watawasumbua.
Unamzungumziaje Rais Magufuli?
Pamoja na kuwa ni mtu anayepigania haki, asiyependa Rushwa na Ubadhilifu lakini kuna watu hata wafanye nini hawachukulii hatua. Kwa nafasi yake hapaswi kuwa na double standards.
Unadhani kuna uhuru wa vyombo vya habari?
Hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Sheria ya Habari ni mbaya kwa wanahabari. Si vema Waziri kupewa uwezo wa kufungia chombo cha habari.
Jecha alifuta uchaguzi kwa ubabe bila kushirikisha wenzake sababu hata katiba ya Zanzibar haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi
Lipumba si mwanachama wa CUF, na Magdalena Sakaya amesimamishwa uanachama, hivyo yote wanayofanya ni batili
Hakuna CUF ya Lipumba au CUF ya Maalim Seif, maamuzi yote ya chama yanafanywa na Baraza Kuu la chama