MAGUFULI Afunguka Kuhusu Mfanyabiashara Aliyeiuza Tanzania Uholanzi, Kufeli kwa Sera Yake ya Sukari..!!


Rais Magufuli alipokuwa akiongea na wafanyabiashara nchini juzi alisema serikali sio kwamba haitaki kushirikiana na sekata binafsi na inatambua mchango wa sekta binafsi kwa uchumi wa nchi

Wafanyabiashara kutokuwa waaminifu
Waziriwa ardhi ametaja compexity kwenye umiliki wa ardhi, amesema kuna wafanyabiashara amabao sio waaminifu na lazima wamuone mchungu Ametolea mfano kuna mfanyabiashara aliyenunua ardhi Tanzania hekta 132,000 na kwenda kuombea mkopo mabenki ya Uholanzi mwaka 2015 na ardhi yenyewe haijaifanyia kazi kabisa
Mfanyabiashara huyo alishirikiana na RUBADA taasisi ya serikali akataka kununua nyingine zaidi ya 300,000 maeneo ya Rufiji akafanye tena hivyo

Pia amesema sekta binafsi wamekuwa na tamaa sana akatolea mfano tenda ya kujenga hosteli za UDSM kuwa walikuwa waijenge kwa bilioni hadi 200 lakini TPBA walijenga kwa bilioni 10 tu

Sukari
Pia amezungumzia sakata la sukari kuwawafanyabiashara walikuwa wanaficha na wakiona demand ya sukari pia imekuwa kubwa mfano kipindi cha mfungo wanapandisha kwa makusudi
Na amedai pia aliwapa wenye viwanda vibali vya kuagiza sukari nje kwa kjuwa wao ndio sukari ya nje inaathiri viwanda vyao lakini wenye viwanda wakaviuza tena vibali kwa wafanyabiashara

Wafanyabiashara kuhujumu kilimo

Rais na waziri mkuu pia amezungumzia wapo wafanyabiashara wanaokuwa wanahujumu kilimo kwa kukopa fedha kwenye benki ya kilimo ambazo serikali ndio imekuwa ikiiwezesha lakini wamekuwa wakifanyia fedha hizo mambo mengine kama kununua malori ya usafirishaji makontena

Alimsusia waziri mkuu wa India
Pia amesema alisusia kwenda kuweka jiwe la msingi kwenye plant ya kufua umeme aliyoambaiwa na waziri mkuu wa India alipokuja kwa sababu waziri mkuu huyo alimchomekea tu alipokuja na terms zao wala hazikujulikana na hakutaka kuiweka nchi kwenye IPTL nyingine

Kuibiwa na makampuni ya madini
Pia amesema makampuni ya madini yanapaswa yaweke hisa zao soko kuu la DSM kwa kuwa wamekuwa hawana accounts za kuzishika wala assets zozote mkiingia kwenye dispute na fedha wanazoleta nchini ni za mshahara tu, na wanakuwa wana declare losses kwenye statement zao na kwenye stock exchange London hisa zao zinafanya vizuri

Ila amesema changamoto za wafanayabiashara amezisikia na atazifanyia kazi na wakikwazwa na mtu serikalini basi wasisite kutaarifu mawaziri wake au yeye na sio kusema serikali ni mbaya

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umeeleweka rais. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad