MAKUSANYO ya Bilioni 76 Yavunja Rekodi Wizara ya Ardhi..!!!


Serikali imefanikiwa kukusanya Sh76bilioni cha makusanyo ya kodi ya pango la ardhi hadi kufikia tarehe 13 Mei 2017 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa.

Akiongea katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,   Dk Yamungu Kayandabila amesema kiwango cha makusanyo ya kodi ya ardhi hakijawahi kufikiwa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa Wizara imekusanya Sh76 bilioni cha kodi ya pango la ardhi.

 “Juhudi za kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa viwanja vilivyopimwa zinaendelea vizuri licha ya changamoto iliyopo hususan mwamko wa wananchi katika kulipa kodi.” amesema Dkt. Kayandabila.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad