Kuna mambo mapya yanayozidi kujitokeza tangu rais Magufuli awasimamishe maafisa wakuu wa Taasisi ya TMAA inayosimamia MADINI ambayo pia ilimfanya rais Magufuli kumvua Uwaziri Mh.Muhongo kama Waziri wa Madini kwa sababu zilizo wazi.
Inavyosemekana ni kuwa mwaka wa 2009 TUME maalumu iliyojulikana kama PRESIDENTIAL MINING REVIEW COMMISSION,iliyoongozwa na JAJI Mark Bomani. Tume hii ilitoa MAPENDEKEZO kuwa SMELTER ijengwe hapa nchini.
Lakini cha kushangaza ni kuwa maafisa hao wa TMAA wakawa tayari wamekuwa COMPROMISED na Makampuni husika yaani WAKAHONGWA ili WANAYAMAZISHE matakwa ya Tanzania Kuwa na UWEZO wake na TEKNLOJIA HIYO.
Katika mbinu zao za kuzima ripoti na mapendekezo ya tume TMAA, miaka sita iliyopita hivi wakaanza mipango ya KUYAMWAGIA MAJI mapendekezo YOTE ya Tume ya Jaji Mark Bomani ili KUIDHOOFISHA kabisa
Na mwishowe KUZIZIMA kabisa NDOTO za Watanzania kuwa na mitambo yao ya SMELTER.
Na hivyo KUTUSALITI sawasawa ili tuendelee KUIBIWA VIZURI na hayo Makampuni.
Mwaka wa 2011 MAAFISA wa TMAA walitembelea miji ya TOKYO na SAGANOSEKI Copper concentrate Smelter nchini JAPAN ili WAJIONEE wenyewe TEKNOLOJIA hiyo na jinsi nchi yetu inavyoweza KUJIJENGEA Smelter yake yenyewe.
Katika safari yao ilikuwa pia wajue GHARAMA za UWEKEZAJI/UJENZI na uwezo na gharama za uendeshaji nchini.
Ikikikumbuka kuwa tume ya Jaji Mark Bomani ilikuwa pia imeenda huko kabla wakati ikiandika na kuchukuwa DATA, ili kutayarisha ripoti mpya ya sheria ya MINIMG LAW/Sheria mpya za MADINI.
Mwaka 2011 TMAA nao wakatoa ripoti yao iliyojulikana kama:
"A STUDY on VIABILITY to CONSTRUCTING a COPPER Concentrate SMELTER in Tanzania"
Ripoti yao ILIPINGA VIKALI mapendekezo ya Tume ya Jaji Bomani.
Na hivyo Kuwaachia wezi field day ya kuiba mchanga wetu WATAKAVYO na WAPENDAVYO. Maana tayari TMAA walikuwa wamekuwa compromised/WAMEHONGWA.
Kwa wale wanaolaumu uamuzi wa Rais Magufuli na kupendelea Makampuni wanaposikia haya si WAONE HUZUNI kuwa hakika TULIIBIWA Vya KUTOSHA na IMETOSHA?
Na Tanzania INAWEZA kabisa KUJIJENGEA yenyewe hiyo MITAMBO.
Maana NIA TUNAYO na UWEZO TUNAO tukishikana pamoja na kushirikiana kama Watanzania
HAKUNA lolote ambalo Tanzania HAITALIWEZA KULIFANYA.
Kwa Maafisa kama hawa wa TMAA WALIOTUSALITI wanastahili kuwa JELA bila HURUMA.
Hatuwezi kuwa taifa la OMBAOMBA wakati kila RASLIMALI tunayo.
Na hali watu wachache wenye tamaa wanataka tubaki Maskini huku wao wakijenga magorofa
TUNAKATAA kama Watanzania.
Mungu IBARIKI Tanzania na Rais Magufuli.
Chanzo: The EastAfrican.
Hao wanaotisha watu ndio hao hao wanaoiweka Tanzania iendeleee kuwa masikini katika ramani ya ulimwengu. Alafu bado ni tupo wote humo humo katika nchi masikini. Hata wakitoka na kuenda manchi yaliyoendelea lakini sio kwao. wataendelea onekana ni wageni tu. Na kuulizwa wanatokea wapi? Pamoja na mahela yao ya usaliti ya kuongwa. kwani ni vijihela kidogo. Si sawa na vijihela wanayochukua hao waliowaonga vijihela vya mifukoni tu. Tena nchi za watu walaaa hawatambuliki na vijihela vya vya kuhongwa wanadhalaulika tu. kwamba hawa watu weusi wanakimbia kwao ni masikini.
ReplyDelete