Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick ambaye jana Rais Magufuli amekubali ombi lake la kujiuzulu katika nafasi yake hiyo amefunguka na kusema katika maisha yake anaumizwa sana pale anapotaka kufanya jambo lakini akakwamishwa na mtu.
Meck Sadick anasema hawezi kuweka wazi sababu kubwa iliyopelekea yeye kuomba kuacha kazi hiyo kwani tayari alishazisema kwa Rais Magufuli ambaye ameamua kukubaliana naye na sasa anasema haitaji kuajiriwa na mtu bali atarudi kwao Usukumani kulima.
"Sababu za kuacha kazi anazijua Rais niliyemuomba, siwezi kumtangazia kila mtu hili, ila changamoto kubwa ni pale unapotaka kitu fulani kifanyike na hakifanyiki kwa hiyo hiki ni kitu kinachotuumiza sana viongozi kwa mfano utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na wananchi wana matarajio kwamba itakapofika 2020 serikali ya CCM itakuwa imefanya moja, mbili, tatu nne sasa yasipofikia hayo ni changamoto kwa kweli kubwa kwa hiyo ndiyo changamoto naweza kusema zinakwamisha maendeleo yetu" alisema Meck Sadick
Mbali na hilo Meck Sadick anasema saizi anarudi Usukumani kulima
"Mimi kazi nayoifahamu ni kilimo ukiachilia mbali hii kazi ya Utawala na kilimo tu kwa hiyo saizi mimi narudi usukumani kwenda kulima, sitegemei kuajiriwa na mtu tena mimi nakwenda kufanya shughuli za kilimo sababu ndiyo nina uzoefu nayo" alisema Meck Sadick