‘Tuna takriban vyuo vikuu 14 na asilimia 90 ya watu wamekwenda shule, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi barani Afrika’ huku akiongezea kwamba uchumi wao unaendelea kuimarika.
Hata hivyo Rais Mugabe amekana madai kwamba taifa hilo lina hali tete.
Zimbabwe imekuwa ikishindwa kuwalipa wafanyikazi wa serikali na huku ikiwekwa katika nafasi ya 24 kulingana na ripoti ya shirika la umoja wa mataifa UNDP, ya maendeleo barani Afrika.