NASISITIZA: Tusijifananishe na Rwanda, Siyo Saizi Yetu Kabisaaa...!!


Unakuta mtu analeta mada za ajabu juu ya ulinganifu wa Tanzania na Rwanda kimaeendeleo!
Huku ni kufikiri sawa kweli?

Ni sawa na kulinganisha usafi wa nyumbani kwangu na usafi wa kijiji chetu, baada ya hapo nikaanza kujisifia eti mimi niko vizuri hapa kwangu kwani nimemshinda Mwenyekiti wa kijiji kwa usafi.
Ndugu zangu kwa wale msioijua Rwanda vizuri; ni nchi ndogo mno! 
Sawa na mkoa mmoja au baadhi ya wilaya moja kubwa!

Huku kutakuwa ni kukosea shabaha sana kujaribu kufanya maendeleo kwa mtazamo wa kile Rwanda wanachofanya!

Kimsingi kwa wao watakuwa sahihi kulingana na mazingira yao, ila sisi tutakuwa tumekosea sana!

Hata kama sisi tungekuwa tumeendelea kuliko wao; endapo wao wangetaka kututazama sisi wangekuwa wanakosea sana!
Tanzania ina rasirimali nyingi kuliko Rwanda hivyo hawawezi kujifananisha na sisi kivyovyote vile.
Tunafanana rangi tu! lakini mazingira yetu ya kiuchumi na wao ni tofauti sana!
Nchi ambazo zinapaswa kujifunza toka kwa Rwanda hapa afrika mashariki ni Burundi, Uganda na pengine na Sudani ya kusini.

Sisi tunazo baadhi ya nchi za kuzitama hapa afrika ila sio za aina ya Rwanda.
Kama Kenya tu kujilinganisha nayo ni uzembe, na aibu kubwa kwetu! itakuwa Rwanda?

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe mwandishi wa mada hii unalako jambo. Usafi ni usafi tu. Ukiwa msafi wa eka moja utakuwa msafi wa eka mia moja. Achana na siasa. Vipi rushwa !! Rwanda hakuna rushwa ata chembe na Tanzania nako jaza mwenyewe. Achana maneno fanya kazi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad