NOMA Sana..Wakati Watu Wakipiga Kelele..Serikali ya JPM Yashusha Bongo Kivuko Hiki Kipya Kimya Kimya..!!!


 Kivuko cha Mv Kazi  kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari kwa mara ya kwanza leo (Jumatatu) baada ya matengenezo kukamilika.

Majaribio hayo yamefanyika kulingana na sheria na utaratibu wa vyombo vya majini ambayo inavitaka kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora.

Awali, wataalamu kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) walipima ubora na uimara wa kivuko hicho kwa kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko na magunia ya mchanga ili kupima uwezo wa kivuko kulingana na mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na mizigo.

Taarifa ya Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) imesema kazi hiyo ilifanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko hakilali upande mmoja na kilionyesha kivuko kiko sawa. Taarifa ya kazi hiyo itakuwa sehemu ya vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa kivuko.

Miongoni mwa waliokuwapo kushuhudia majaribio hayo alikuwa mkuu wa vivuko Magogoni/Kigamboni, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwa kuwa kitawasaidia kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa asubuhi na jioni.

Kivuko hicho kitaongeza idadi ya vivuko kufikia vitatu vitakavyotoa huduma ya kuvusha abiria na magari katika eneo la Magogoni/Kigamboni.

Ujenzi wa kivuko cha Mv Kazi umegharimu Sh7.3 bilioni na kina uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 sawa na jumla ya tani 170. Kivuko hicho kitakabidhiwa rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) kwa ajili ya kuanza kutoa huduma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad