PAPA Francis Atoa Ya Moyoni Mgogoro Wa Marekani Na Korea..!!!


Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis ametaka mjadala wa kimataifa uandaliwe wa kususluhisha mvutano unaozidi kutokota kati ya Marekani na Korea kaskazini akisema kwamba swala hilo limekuwa kaa la moto.

Papa Francis amewaambia wanahabari kwamba mzozo baina ya mataifa hayo huenda ukazua vita vitakavyoangamiza watu wengi.

Awali manowari ya kivita ya Marekani iliwasili karibu na rasi ya Korea, saa chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kombora ambalo lilitibuka.

Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumua Korea Kaskazini kwa kuiokosea heshima jirani wake China na rais wake.

Hivi majuzi Trump alimulika rais wa China Xi Jinping na kumpongeza kwa kujitahidi kutatua mzozo wa Korea Kaskazini.

Jaribo la kombora la Korea Kaskazini lilijiri saa chache baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kujadili mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbona hasemi ya palestina na Israel.
    roho za makafiri ni tamu kuliko waislamu.sote ni binadamu tutarudi tu kwa MUNGU MMOJA ASIE NA USHIRIKA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad