POLEPOLE Aaanza Tumbua Tumbua Ndani ya CCM..Afyeka Vigogo Hawa 20 Harakaharaka..!!!


VIONGOZI zaidi ya 20 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya kata na matawi Jijini Arusha wamesimamishwa uongozi kwa tuhuma za kufuja mali za chama.

Kata ambazo viongozi wake wamesimamishwa kwa tuhuma hizo za ubadhirifu ni Unga Limited, Themi, Sekei, Sombetini na Daraja Mbili. Viongozi hao ni wenyeviti, makatibu, wachumi na makatibu wenezi.

Katika kata ya Unga Limited, mbali ya viongozi wa kata kuchukuliwa hatua pia viongozi wa matawi wa wamesimamishwa kwa madai ya kushindwa kusimamia ipasavyo mali za chama.

Mbali ya tuhuma za kufuja mali za chama, baadhi ya viongozi hao pia wanatuhumiwa kufanya hujuma katika chaguzi zilizopita, ikiwa ni pamoja na kuficha fomu kwa wanachama wanaotaka kuwania uongozi ili wao waweze kuwania tena nafasi hizo na kupita bila ya kupingwa ama kuwa na wagombea dhaifu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Humphrey Pole pole alisema na kutoa salamu kwa watendaji wote wa chama hicho kote nchini kuhakikisha wanatunza mali na kuzitumia kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.

Polepole alisema katika baadhi ya maeneo mali za chama zinatafunwa kama mchwa na viongozi mbalimbali hivyo msako unaendelea kote nchini kuwasaka na bila ya kuonea mtu.

Katibu huyo alisema chama hakiwezi kuwavumilia viongozi wanaofuja mali kwa sasa chini ya uenyekiti wa Rais John Magufuli. "Wote watachukuliwa hatua kali," alisema.

"Kuna baadhi ya maeneo mali za chama zinatumika vizuri sana... kuna baadhi ya maeneo mengine viongozi wanafuja vibaya lakini wameachwa.
"Kwa sasa hilo halipo.

"Heri kuwa na viongozi wachache waaminifu na waadilifu wenye kufuata katiba ya chama kuliko kuwa na utitiri wa viongozi wezi na wasiokuwa waaminfu. Hilo haliko kwa sasa chini ya uongozi wa (Rais) Magufuli."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad