Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekemea vikali mauaji yanayotokea mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Alhamisi Polepole amesema kuwa kama CCM wanataka kuona mauaji hayo yanaendelea kukemewa zaidi.
Polepole ameonyesha masikitiko yake kwa vyama vya upinzani kukaa kimya badala ya kuungana kama Taifa kukemea mauaji ya watendaji wa CCM yanayoendelea mkoani Pwani.
"Kuungana kwenye ruzuku, hapana vyama vinapaswa kuwa na umoja katika masuala mbalimbali ikiwamo mauaji hayo," amesema Polepole.