MAGARI matano kati ya 16 yaliyofanyiwa ukaguzi mwishoni mwa wiki na askari wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Kipolisi Tarime-Rorya wakati ukaguzi wa magari ya kubebea wanafaunzi yamebainika kutokuwa na ubora na viwango vya kubeba wanafunzi.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Tarime-Rorya, Joseph Bukombe alisema kasoro zilizobainika ni pamoja na kuwa na ubovu mkubwa na mengine yanadaiwa kutoka nchi ya jirani ya Kenya na kuingia Tarime kubeba wanafunzi, huku yakikwepa kodi.
“Tumeamua kuwaita wamiliki wa shule katika wilaya zetu hizi wenye magari ya kubeba wanafunzi kuleta magari yao hapa kwa ajili ya ukaguzi ambapo magari tano kati ya 16 tuliyoyakagua hapa leo (jana), yamebainika kuwa yana ubovu mkubwa yakiwemo yaliyofungwa kamba kwenye injini na giaboksi, yaliyooza bodi zake , kutokuwa na taa , wepa , matairi mabovu , viti vilivyochakaa,”alisema.
Alisema walikuta gari lingine likiwa na namba za usajili wa Kenya, likiwa limechakaa bodi yake tumeyatoa namba zake na mengine ambayo yamebainika na ubovu mdogo yatapigwa faini na kwamba wengine wamewaonya ili wayafanyie magari yao matengenezo.
Alitaja magari matano yaliyofanyiwa ukaguzi na kubainika kuwa yana ubovu mkubwa kuwa ni lenye namba za usajili T 277 APU la Shule ya Mwera Vision iliyopo Tarime mjini, lenye namba T 721 BFH kutoka shule ya sekondari Angel House na lenye namba T 444 AAR la shule ya ST Jude ya Buhemba, Tarime.
Gari lingine ni lenye namba za usajili T 861 DHM la shule ya awali na msingi ya Maryo, Nyamongo na gari lenye namba za usajili wa Kenya K AZ 088 R aina ya Nissan UD ambalo bodi yake ni mbovu, imechakaa huku likiendelea kutumia namba za usajili za nchi hiyo bila kubadilishwa.
Magari mengine yaliyokaguliwa na kukutwa na ubovu kidogo na kupigwa faini ni lenye namba za usajili T 652 DBV kutoka Shule ya Angel House, T 199 CRW kutoka Shule ya Remagwe, T 125 ZCU kutoka Shule ya Gwitiryo , T 903 BGM kutoka shule ya Msati Hill ya mjini Tarime, T 981 DFB kutoka shule ya Bustani RC Tarime , T 938 DFQ kutoka shule ya Elizabeth Memoriam , T 378 DEH kutoka Shule ya MT Mikael Maria Gamasara na T 422 DHV kutoka Shule ya Msati Hill Crest ya mj