RASMI...Mzee Mkapa Afunguka Haya ya Moyoni Kuhusu Serikali ya JPM..Anyooshea Kidole Sakata la Kufukuza Wenye Vyeti Feki..!!!


Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa kwa mara ya kwanza amezungumzia utawala wa Rais Dkt John Pombe Magufuli huku akimpongeza utendaji kazi wake unavyokwenda.

Rais Mkapa alimpongeza kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti vya kughushi vya taaluma na kazi, na akasema anasikitika tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.

Mzee Mkapa aliyesema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo yake na Shirika la Habari la Ujerumani (DW) ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumzia ni utawala wa Rais Magufuli, uhuru wa vyombo vya habari, masuala ya uchumi.

Alisema Mkapa kuwa, wenye vyeti feki au watumishi hewa walikuwa wakiingizia serikali hasara wengine wakiendelea kukaa madarakani bila ya kustaafu, hivyo lilikuwa ni jambo la lazima kufanyika ni kwa manufaa ya taifa.

“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga mkono kabisa,” alisema Mkapa.

Kauli hii ya Rais Mkapa imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt Magufuli kuwaamuru watumishi wa umma 9,932 waondoke kwenye utumishi wao baada ya kubainika kughushi vyati vyao.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwa hayo kweli kafanya kazi nzuri sana lakini kitu kimmoja nashanga sana paul makonda ambae hata jona sio lake (daudi bashite) kila kitu feki kazi pia anatumia nguvu ????? mbona hakutolewa madarakani au RC NI KAZI YA PRIVATE SECTOR KWA HAPO KUNA WALAKINI HAIWEZEKANI WASEME KAZI YA MKUU WA MKOA INATAKIWA AJUE KUSOMA NA KUANDIKA KAMA NI HIVO TUKO WENGI TUJE TUTAPEWA KAZI?

    ReplyDelete
  2. ni kazi kubwa na safi sana lakini kuna kitu alivho haribu hivo nchi gani duniani itaajiri mkuu wa mkoa ambae na jua kusoma na kiandika tu jamani hii kweli yaingia akili? hivo mie muuza sokoni najua kuandika na kusoma na najua kuendeaha nchi kweli nijaribu utanipa ajira? mbona tanzania tumeheuka vichekesho PAUL MAKONDA ambae anaitwa daudi bashite tunataka kujua uhakiki wake kwa kina na kwa nini Rais ana defend kuliko kawaida kuna nini kinacho endelea?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad