RASMI..TRA Washusha Rungu la Kodi kwa Wamachinga..Yawataka Kuanza Kulipa Kodi..!!!


MAMLAKA ya MapatoTanzania (TRA) imetangaza mkakati wa kuanza kuwasajili wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga ili waweze kutambulika na kurasimishwa rasmi.

Mkurugenzi wa Elimu Kwa Walipa Kodi, Richard Kayombo, akizungumza katika semina ya waandishi wa habari jana amesema wamachinga baada ya kutambuliwa watawekewa utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao na kuchangia mapato Kwa serikali.

Kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), amesema TRA haitozi Kodi Kwa mizigo inayosafirishwa kwenda nje ya nchi badala yake mizigo hiyo inatozwa Kwa huduma zinazofanyika nchini.

Mada zilizojadiliwa ktk semina hiyo ni Kodi ya Majengo na elimu ya Kodi Kwa anayeanza biashara.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad