RAY C - Naliaga Nikiambiwa Wimbo Wangu Mbaya..!!!


Msanii mkongwe anayetamba kwa sasa na wimbo wa 'Unanimaliza', Rehema Chalamila ' Ray C'  amefunguka kuwa machozi huwa yanamdondoka pindi anapomsikilizisha mtu wimbo ambao anaamini utafanya vizuri alafu akajibiwa hautokuwa 'hit'.

Ray C amefunguka hayo leo kwenye Planet Bongo wakati akitambulisha wimbo wake mpya na kueleza kuwa kabla hajapeleka wimbo kwenye Radio huwa anasikilizisha watu na anapopata majibu tofauti na alivyofikiria huwa yanamuumiza na kumfanya atengeneze ngoma nyingine  kali akiwa na machozi.

"Kabla sijatoa  wimbo nina tabia ya kuwasikilizisha watu wa chache ambao naamini wana sikio la muziki. Huwa sichukii nikiambiwa wimbo ni mbaya lakini machozi huwa yananitoka kwa sababu mimi naamini nimetengeneza hit alafu mtu anakwambia hamna kitu. Hata huu wimbo wa unanimaliza ndio ulipita kati ya nyimbo tano nilizotengeneza na nyingine zilizobaki wamenishauri nisiziweke kwenye albam"- Ray C alifunguka.

Aidha Ray C amewataka wasanii wengine kutojiamini kupitiliza kiasi cha kuchukua wimbo studio na kuupeleka kwa mashabiki  pasipokupata ushauri kwani kufanya hivyo  ndicho chanzo cha nyimbo kupoteza ladha mapema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad