Riyama Alia na Umaskini wa Bongo Movies


Msanii wa bongo movie Riyama Ally amefunguka na kusema licha ya kufanya kazi ya filamu kwa miaka zaidi ya 15 lakini hajapata mafanikio yale ambayo watu wanategemea angekuwa nayo kutokana na uwezo wake wa kuigiza.

Rihaya Ally alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live na kusema hakuna kitu kinaumiza kama unapofanya biashara na kulipa kodi halafu mshindani wako ambaye anafanya biashara hiyo hiyo anafanya mambo kinyume halipi kodi, kazi yake ni kufyatua tu filamu na kuziingiza sokoni.

"Kikawaida changamoto katika biashara ni nyingi na hakuna biashara ambayo haina leseni au haulipi kodi, na kikawaida kila jambo linafanyika katika misingi ya sheria hatuwezi kufanya kitu kinyume cha sheria, kwa hiyo sisi tunalipa kodi halafu wenzetu inakuwa tu wanafyatua filamu bila kulipa kodi, hiyo inaumiza sana sababu mimi nipo kwenye game kwa zaidi ya miaka 15 sina baiskeli, sina bajaji, sina gari sina chochote"  alisema Riyama Ally

Mbali na hilo Riyama Ally anasema wasanii wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na mambo kama hayo, ila anawataka wasanii wa bongo kujipanga na kutengeneza filamu ambazo wananchi wanazihitaji na kusema kuzuia filamu za nje zisiingie ni jambo la ajabu

"Kutokana na mambo hayo hayo wasanii wengi wanashinda kufanikiwa lakini kama wenzetu wangekuwa wanalipa kodi kama sisi basi hakuna tatizo, kama ukiwa msanii mzuri na unakidhi mahitaji ya jamii huwezi kuhofia kazi za nje maana hizo ndiyo kioo chetu sisi, wenzetu wametutangulia sana inabidi tujifunze kupitia wao, kwa hiyo zinatakiwa kuendelea kuingia lakini kwa kufuata utaratibu ili na kazi zao nao zilipiwe kodi nchini" alisisitiza Riyama

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad