Sababu za Issa Makamba wa Serengeti Boys kurudishwa Tanzania

Tumepata nafasi ya kuongea na Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas akiwa Gabon kuhusiana na nahodha wa timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys Issa Abdi Makamba.

Makamba akiwa mazoezini aliumia siku tatu kabla ya kuanzia kwa mashindano ya AFCON U-17 hivyo jina lake likaondolewa katika orodha ya Wachezaji wa Serengeti Boys watakaoshiriki michuano hiyo japokua aliendelea kubaki kambini na timu.

Taarifa za uhakika ni kwamba leo amerudishwa Tanzania licha ya kuwa awali viongozi walisema atakuwa na wenzake hadi mwisho wa mashindano, ni nini kilichofanya arudishwe Tanzania? afisa habari wa TFF Alfred Lucas ameongea haya:

“Ni kweli amerejea nyumbani na kilichofanya arudishwe ni sababu kuu mbili za Madaktari watatu, CAF walileta mchezo mmoja Port Gentil na yeye kwa hali yake haipaswa asafiri hivyo inakua kama kumsumbua zaidi” 

‘Sababu nyingine ni kwamba anapoendelea kubaki na Wachezaji wenzake na kuhudhuria mechi akiwa benchi inazidi kumuumiza zaidi sababu anatamani angekua anacheza, Madaktari wameshauri arudishwe tu Tanzania’
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad