Sakata la Diamond Kudaiwa Mil 400 na TRA lafika Hapa


Siku chache tangu Mbunge wa Jimbo la Mikumi Professa Jay kupaza sauti yake kuhusu makadirio makubwa ya kodi anayotakiwa kulipa Mwanamke anayewika nje na ndani ya nchi  katika muziki wa bongo Flavor Diamond  Platnum Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imekanusha kumlipisha kwa makadirio nyota huyo. 
  

Mkurugenzi  wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nassib Abdul ( Diamond Platnamuz) kulipa kodi ya shilingi Milioni 400. 

Hayo ameyasema leo wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa waaandishi. 

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kiasi kodi anayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,”, 

“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” amesema Kayombo. 

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sh mil mia 4 au 8 kwa dimond siyo tatizo. Anamiliki gari pekee Tanzania RR itakuwa hii. J3 anawaungisha TRA na bila swali lolote. Tungojeni tumawasiliana na Sallam na mambo ni poa tu.

    ReplyDelete
  2. Kujionyesha sana kutakumaliza kaka. TRA inakamua hata Wamachinga.WEWE ungebakia vile vile kwenu Mbagala TRA Wangekuacha.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad