Serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) itaisaidia serikali ya jimbo la Puntland la Somalia kuboresha sekta yake ya utumishi wa umma kwa kuendesha mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa umma wa jimbo hilo.
Puntland ni Jimbo la Kusini mwa Somalia ambalo limejitangazia mamlaka yake ya ndani, ingawa halitaki kujitenga moja kwa moja na Somalia yenye machafuko.
Mkataba wa makubaliano hayo ulisainiwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angela Kairuki na Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Puntland, Abdurahman Ahmed Abdulle.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo TPSC itashirikiana na Chuo Kikuu Cha Puntland kuendesha kozi mbalimbali kwa watumishi wa umma wa Puntland hususani za muda mfupi na watumishi wengi wa umma wa jimbo hilo watanufaika na programu kadhaa za mafunzo.
Mpango huo wa Puntland umefadhiliwa na Benki ya Dunia ambao pia umeuwezesha ujumbe wa Puntland kuzuru Tanzania mara kadhaa kwa lengo la kufanikisha makubaliano hayo.
Waziri Kairuki alisema makubaliano hayo yanalenga kuboresha uhusiano wa watu wa Tanzania na Puntland na yatasaidia kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa Umma wa Jimbo la Puntland.
Kwa mujibu wa Kairuki, Tanzania kupitia chuo cha Utumishi wa Umma kimekuwa kikishirikiana na taasisi za ndani na nje kuboresha sekta ya umma.
Kwa upande wake Waziri Abdulle alisema jimbo lake limechagua kuja kujifunza Tanzania kutokana na umadhubuti wake katika sekta ya utumishi wa Umma.
Alisema anaamini mkataba huo utanufaika jimbo lake.
Hongera .!!! Ndiyo mqanzo on the right �� direction
ReplyDelete