SERIKALI Yaeleza Hali Ya Sukari Nchini Kuelekea Mwezi Wa Mtukufu Wa Ramadhan..!!!


Serikali imesema kuwa iko macho kuhusiana na suala la sukari nchini na inafanya jitihada zote ili kupata mahitaji yote wakati mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukikaribia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma na kudai kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 ambapo kwa hapa nchini tani 320,000 zinazalishwa na hivyo mwaka huu imeagiza sukari tani 80,000 na tayari tani 35,000 zimeshaingia nchini.

Majaliwa amewataka Watanzania kushirikiana katika kuwasihi wafanyabiashara kushusha bei ya sukari ambayo wameipandisha hivi sasa.

Waziri Mkuu, Majaliwa amesema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge, Jakuh Hashim Ayoub aliyemuuliza kuhusu mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kwamba kuna tatizo la sukari huku wananchi wakihiwa na uhitaji na kwamba hivi asa zipo tani 100,000 tu za sukari.

Mhe. Ayoub amesema kuwa sukari iliyoagizwa kwa watu waliopewa vibali vya sukari itakuwa imekwisha wakati mwezi mtukufu wa Ramadhan utakapoanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad