Moja kati ya benki kubwa nchini Tanzania, FBME, imenyang’anywa leseni na kufungiwa huduma kutokana na kuhusishwa na kusaidia kutoa fedha kwa taasisi ya kigaidi ya Hezbollah.
Benki ya FBME, zamani Federal Bank of The Middle East, ilikua na makao makuu yake nchini Cyprus kabla ya kuhamisha rasmi nchini Tanzania mwaka 2003.
Tanzania imelazimika kufuta leseni ya uendeshaji wa benki hiyo kufuatia ripoti za kiinteligensia kutoka kwa serikali ya Marekani, ambayo ilikua ikiendesha uchunguzi dhidi ya benki hiyo tangu mwaka 2014.
FBME inasadikiwa kuwa miongoni mwa benki kubwa nchini Tanzania yenye mtaji wa zaidi ya dola bilioni 4.