SHAMBULIO la Kigaidi Laua 19 Katika Tamasha la Muziki Uingereza..!!!


Watu 19 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa baada ya bomu kulipua ukumbi wa tamasha la muziki, katika mji wa Manchester, Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.

Iwapo shambulio hilo litathibitishwa kuwa ni la kigaidi, linatajwa kuwa ni baya zaidi kuwahi kuikumba Uinereza.

 Shambulio kubwa zaidi lilitokea Julai 2005 ambapo watu zaidi ya 50 walipoteza maisha baada ya kutokea mlipuko, jijini London.

Katika tukio la jana, mashuhuda wanasema shambulio hilo lilitokea mara tu baada ya mwanamuziki wa Marekani Ariana Grande kumaliza kuwatumbuiza mashabiki wake.

Mashudhuda  wa tukio hilo wamesema waliona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya  mabomu.

Eneo kulikotokea mulipuko huo limezingirwa na polisi waliojihami wanaendelea kushika doria.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad