Shamsa amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kukerwa muda mrefu na watu wanaopenda kutumia mitandao ya kijamii kuanzisha mijadala ambayo haina ukweli wowote wala kuwa na taswira nzuri katika jamii.
"Nina imani hii mitandao tungeitumia vizuri tungekuwa na maendeleo makubwa,ila unavyotumika jamani ni kero. Sisi wabongo ni kiboko aise, wabongo wa instagram ni kiboko Wallah, mtu anaweza akatengeneza jambo likafanana na ukweli mpaka mwenyewe ukachoka. Wabongo tuna vipaji" aliandika Shamsa.