Kwanini serikali inapenda kusema uongo hata kwa mambo yaliyo wazi? Waziri wa fedha amesema kuwa sarafu yetu (shilingi) imezidi kuimarika dhidi ya dola kwa mwaka huu wa fedha unaoishia. Huu ni uongo wa wazi kabisa. Ukweli ni kwamba shilingi imezidi kuporomoka maradufu dhidi ya dola kwa kipindi cha mwaka huu wa fedha.
Kwa mujibu wa records za BOT, tarehe 1 July mwaka jana thamani ya dola moja ya Marekani ilikua sawa na TZS 2,126.07/= (bei ya kuuzia), leo tarehe 29 mwezi May 2017, dola moja ya Marekani ni sawa na TZS 2,280.80/= (bei ya kuuzia). This means sarafu yetu imeporomoka kwa 7.2% dhidi ya dola ya kimarekani.
Sasa Waziri Mpango anaposema sarafu imeimarika anamaanisha nini? Uongo huu ni kwa faida ya nani? Kama serikali inaweza kusema UONGO kwenye mambo yaliyo wazi kama haya, vp kwa yale yasiyo wazi?? Kwanini mnatafuta credit kwa kusema uongo? Mkisema ukweli mtapoteza nini? Shame on u.!!