SIMBA Maji ya Shingo...Wakubali tu Kombe ni la Yanga Msimu Huu


Si vibaya ukisema wamekubali kiana! 

Maana kipigo cha mabao 2-1 walichokitoa Yanga kwa Mbeya City kinawafanya wabakize ushindi wa mechi moja tu kubeba ubingwa na kesho wanacheza dhidi ya Toto African jijini Dar es Salaam. 

Watani wao Simba sasa wanaonekana kukubali kwamba hawana ujanja wa kuwazuia Yanga ambao ni mabingwa watetezi kubeba tena ubingwa. 

Kama Yanga wakiutwaa ubingwa msimu huu, maana yake ni kwamba watakuwa wameutwaa kwa mara ya tatu mfululizo, na kuleta tafsiri kwamba wametawala soka la Tanzania kwa sasa. 

Yanga ilirejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kuichapa Mbeya City mabao 2-1. Imefikisha pointi 65 sawa na Simba lakini imebakiza michezo miwili wakati Msimbazi wamebakiza mchezo mmoja. 

Kwa michezo ambayo Yanga imebakiza dhidi ya Toto na Mbao, hata kama itapoteza mchezo mmojawapo, halafu ikashinda mwingine, na Simba kupewa pointi tatu za mezani ilizopanga kuzifukuzia Fifa, Yanga bado watakuwa mabingwa kwa kuwa wana uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. 

Kama kwa vyovyote vile wakilingana pointi, Simba italazimika ishinde mabao kuanzia 11-0 katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui jijini Dar. 

Yanga ambayo juzi Jumamosi iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City, kwa sasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 65 sawa na Simba, lakini ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. 

Kesho Jumanne, Yanga itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, na kama ikiibuka na ushindi, basi itatangaza ubingwa kwani itakuwa imeiacha Simba kwa pointi tatu nyuma, huku timu zote zikibakiwa na mchezo mmojammoja. 
Mayanja amesema walikuwa wakisubiri kuona Yanga wakiteleza mbele ya Mbeya City, lakini matokeo ya ushindi waliyoyapata yanawafanya kuamini kwamba wapinzani wao hao wanaenda kuwa mabingwa. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad