SIMBA Sc Vs Mbao FC Kuchezwa Dodoma..!!!!


Mchezo wa Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup HD – ASFC), kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza, utafanyika Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 ya michuano ya ASFC kuhusu Uwanja wa mashindano inasema: “Uwanja wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD utakuwa ni uwanja wenye hadhi inayokubalika na TFF.”

Wakati huo huo ligi kuu ya Tanzania Bara, itarendelea Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu  kwa jumla ya michezo sita.

Kwa mujjibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na mechi moja.

Michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wakati mechi zote zitaanza saa 10.00 jioni, mchezo kati ya Azam na Mbao utaanza saa 1.00 usiku.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad