SIMBA Waipigia Saluti Yanga..Wakubali Kushindwa Ligi Kuu!!!!


MAKAMU wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amewapongeza mahasimu wao Yanga, kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na kusema wanajipanga kwa msimu ujao.

Simba imeshindwa kumaliza vizuri ligi ya msimu huu, baada ya kuongoza kwa tofauti ya pointi nane kwa muda mrefu hadi ilipokuja kuenguliwa kileleni kufuatia kipigo cha mabao 2-1, kutoka kwa Kagera Sugar.

Akizungumza  jana, Kaburu alisema wanajisikia vibaya kuukosa ubingwa wa msimu huu, lakini hawana budi kuwapongeza Yanga kutokana na kufanikiwa kutetea taji hilo kwa bahati dakika za mwisho.

“Yanga ni wapinzani wetu kwenye ligi ya Tanzania, tunawapongeza kwa taji hilo lakini ni bahati ndiyo imewabeba kwa sababu karibu msimu mzima sisi ndiyo tumeongoza ligi lakini mwishoni tuliharibu na wenzetu kupata nafasi,” alisema Kaburu.

Kiongozi huyo alisema baada ya kupoteza taji hilo nguvu zao kwa sasa wamezielekeza kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA, dhidi ya Mbao FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma Mei 28 mwaka huu.

Yanga inaongoza msimamo ikiwa na pointi 63 na Simba ina pointi 65 huku kila mmoja akibakiwa na mechi moja. Ili Simba itwae ubingwa inahitaji kuomba Mbao iifunge Yanga mabao 5-0 katika mechi ya mwisho huku yenyewe ikiifunga Mwadui mabao 8-0 jambo ambalo kwa mwenendo wa ligi ulivyo halitawezekana.

Kaburu alisema wamepanga timu yao kuipeleka Zanzibar kupiga kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo huo wa fainali lengo ni kuhakikisha wanashinda ili kushiriki na michuano ya kimataifa.

Alisema, baada ya mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya Mwadui keshokutwa, kikosi chao kitaondoka Dar es Salaam Jumapili kwa ajili ya kambi hiyo ambayo wanaamini itakuwa na mafanikio kutokana na ari waliyokuwa nayo wachezaji na viongozi.

Huu ni msimu wa nne mfululizo Simba inalikosa taji hilo, na kuwaachia wapinzani wao Yanga wakilitwaa moja kwa moja baada ya kulichukua mara tatu mfululizo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad