SPIKA Ndugai Afunguka Maana ya Tusi 'FALA' Alilotukanwa na Halima Mdee Bungeni..!!!


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai jana ameonyesha aliumizwa na kitendo cha Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Halima Mdee kumwambia 'fala' bungeni na kusema hata kama mtu humpendi lakini si vyema kumtusi matusi.

Job Ndugai alisema hayo alipokuwa akitoa maana ya neno fala bungeni ambapo ilibidi arejee maana hiyo kwa kusoma kupitia kamusi ya Kiswahili ambayo ilitoa maana kuwa fala ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri.

"Kwa neno ambalo alilisema Halima Mdee humu ndani, kamati imeenda kwenye tafsiri ikachukua Kamusi kwa neno lile alilosema ambalo maana yake kwa yule unayemwambia 'Fala' ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri, ni mtu mpumbavu, ni mtu bwege, ni mtu mjinga, ni mtu bozi, ni gulagula. Ndiyo maana nikasema sisi Waafrika hata kama humpendi namna gani mwenzako huwezi kumfanyia hivyo" alisisitiza Job Ndugai 

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukosefu WA Adabu na Malezi Mema. pole Sana inauma. Labda wapiga Kira wake wamemtambua kwa upotefu wao. Huyu so WA kuwa hapo na kujinasibisha kuwa mhesgimiwa. Ni lazima fomu za ubunge zirekebishwe na pipengelee vya ufafanuzi viwekwe vyenye kuzingatia Nidhamu busara na uvumilivu. Na hatua za mkosefu. Hapo ITAKIWA elekevu. Milimonyi mwana!! Mchekulu Ali mzi'mzi WA kupiga mhunde Kali.. HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  2. How how??? How comes...?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad