TAHADHARI...Mvua Kubwa Kuendelea Kunyesha Dar na Ukanda Wote wa Pwani ..!!!!


Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), imesema hali ya vipindi vifupi vya mvua katika maeneo ya mwambao wa pwani ya Kaskazini itaendelea hadi Mei 9.

Taarifa ya tahadhari iliyotolewa na TMA jana inasema kunatarajiwa kuwapo vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24. Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA imesema hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini.

“Wakazi wa maeneo tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki. Mamlaka inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi,” imesema taarifa ya TMA.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad