KUFUATIA tishio la kuwapo kwa ‘software’ yenye virusi aina ya WannaCry, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewatahadharisha watumiaji wa kompyuta kutofungua viambatanishi wasivyovijua kwenye barua pepe zao.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba, amesema kufuatia tishio hilo taasisi zianza kuchukua tahadhari kwa kutunza data (taarifa) nje ya mtandao ili kuepuka athari hizo kama kutatokea kompyuta kusambuliwa na virusi hivyo.
Kilaba amesema tishio la virusi WannaCry haliko kwenye kompyuta pekee bali pia kwenye simu za kisasa endapo utafungua kiambatanisho au link yenye virusi hivyo.
“Endapo mtumiaji au taasisi wanakumbwa na tatizo hilo basi watoe taarifa kwa Timu ya kitaifa ya dharura ya kompyuta (TZCERT),”