TETESI za Uwepo wa Al Shabab Nchini..Mwanafunzi wa Chuo cha St Joseph Akamatwa Akiwa na Bastola Yenye Risasi 13..!!!


Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph,  Lazaro Mbise (23) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la  kukutwa na bastola pamoja na risasi 13 ambayo alimwibia baba yake.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mwanafunzi huyo alipokamatwa alikiri kuiba bastola hiyo pamoja na fedha kiasi cha Sh800, 000.

“Bastola hiyo ni LUGER cz100 mtuhumiwa alikiri aliiba pamoja na risasi kutoka kwa baba yake,” amesema Sirro.

Kamishna Sirro ameagiza mzazi wa mtuhumiwa kukamatwa ili afikishwe mahakamani kwa kosa la kutohifadhi bastola yake vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad