Kampuni ya kuunda magari ya Toyota kutoka Japan imetangaza kuunga mkono kundi la waandisi ambalo linaunda gari linaloruka kwa kufadhili.
Toyota imetoa kiasi cha Dola 300k za Kimarekani kwa kundi hilo ambalo huendesha shughuli zake nje ya mji wa Toyota nchini Japan.
Kundi hilo limekuwa likipata michango kugharamia kuundwa kwa gari hilo linalotumia teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani na linatajwa kuwa gari dogo zaidi linaloruka kuwahi kuundwa.
Uharaka wa kuundwa kwa Gari hilo linalopaa unavaliwa njuga na makampuni mengi nchini Japan kwani matarajio ya kundi hilo la wataalamu wanataka magari hayo yatumike kwenye tukio la kuwasha Mwenge wa Michuano ya olimpiki mwaka 2020 mjini Tokyo,Japan .