TRAFIKI Waliokuwa Zamu Siku ya Ajali ya Wanafunzi Arusha Kuchukuliwa Hatua...!!!!


WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema itawachukulia hatua watu wote walioshindwa kutimiza wajibu wao katika ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32 wa Shule ya Lucky Vincent ya Jijini Arusha.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na kila atakayebainika hakutimiza wajibu wake atachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

Mei 6, mwaka huu, kulitokea ajali kwenye mlima wa Rhotia wakati wanafunzi hao walipokwenda kufanya mitihani ya ujirani mwema katika Shule ya Tumaini Junior iliyopo Wilayani Karatu na kusababisha vifo vya wanafunzi 32.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania: raia wote kwa ujumla wao kukubali sheria za nchi na kuzitii. Wenye kupata ndo wako mstari wa mbele ktk uvunjaji wa sheria za nchi na hongo ndo kipau mbele. Mtu mwenye pesa na mamlaka aliyetenda kosa na kuthibitika Mi makusudi adhabu itolewayo iwe kali na kufirisiwa pia. Waache tabia kukwepa kodi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad