Rais wa Marekani Donald Trump amesema hachunguzwi na mtu yeyote wala shirika la ujasusi la FBI halimchunguzi. Hiyo ni baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la FBI.
Akizungumza na chombo cha habari cha NBC jana, Trump alisema kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.
Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya maofisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.
Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliyopingwa na mrithi wa Comey.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo, Trump aliiambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza Comey iwapo alikuwa akimchunguza.
“Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia, huchunguzwi.” alisema Trump
Chanzo BBC.